Wenyeji Wetu

Ijue MS-TCDC

MS-TCDC ni kituo cha mafunzo kilichopo Usa River, Arusha, Tanzania. Kituo hiki kilianzishwa mwaka 1967 kupitia makubaliano ya kati ya serikali za Denmark na Tanzania, kwa lengo la kukuza maendeleo endelevu na kukuza ushirikiano kati ya nchi za Kiafrika. Kwa upande wa lugha na utamaduni wa Kiswahili, MS-TCDC ni kituo kikubwa zaidi katika Afrika, pengine duniani kote, kifundishacho lugha na utamaduni wa Kiswahili kwa wageni. Kila mwaka, kinapokea wanafunzi wa kigeni watokao Marekani, Ulaya, na kote duniani.

Arusha

Arusha Waijua?

Arusha ni miongoni mwa majiji maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Makao Makuu ya EAC

Arusha ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo inaziunganisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kitovu cha Utalii

Arusha ni kitovu cha Utalii katika nchi ya Tanzania na pako karibu na vivutio vikubwa sana duniani, kama Mlima Kilimanjaro, Serengeti, Ngorongoro, Manyara, na Tarangire.

Geneva ya Afrika

Arusha ni mji unaotambulika kama Geneva ya Afrika kwa sababu ya umuhimu wake katika masuala mbalimbali ya kidplomasia. Pia pako ni katikati ya umbali kutoka Capetown hadi Cairo.

Tunakungoja

Fanya Hima! Tunakungoja Arusha

Ikiwa bado hujajisajili, tafadhali fanya hivyo sasa. Hata kama huwasilishi makala yoyote, tafadhali jisajili ili uweze kushiriki katika kongamano hili la kidunia la kwanza kufanyika jijini Arusha.